Mechi ya Wahariri na Klabu ya Waandishi Iringa sasa rasmi

Kutoka Kulia Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim, Nahodha Msaidizi wa Timu ya Soka ya Wahariri Saleh Mohamed, Nahodha wa timu hiyo Kulwa Karedia na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu wakionesha sehemu ya vifaa mbalimbali vya michezo vilivyotolewa na Vodacom kuwezesha mechi kati ya timu ya Wahariri na Timu ya wanahabari wa Mkoa wa Iringa. Mechi hiyo itachezwa mwishoni mwa wiki mjini Iringa.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akikabidhi kwa Nahodha wa Timu ya Soka ya Wahariri Kulwa Karedia vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya timu yake na ya wanahabari wa mkoa wa Iringa vyenye thamani ya Sh 3 Milioni. Timu mbili hizo zinakutana kwenye mechi ya kirafiki itakayochezwa mjini Iringa mwishoni mwa wiki.Wanaoshuhudia ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(wa kwanza kushoto) na Nahodha Msaidizi Saleh Mohammed
 Nahodha wa timu ya soka ya Wahariri nchini Kulwa Karedia akiongea na waandihsi wa habari(hawapo pichani)muda mfupi kabla ya kupokea vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya timu yake na ya wanahabari wa mkoa wa Iringa vyenye thamani ya Sh 3 Milioni. Timu mbili hizo zinakutana kwenye mechi ya kirafiki itakayochezwa mjini Iringa mwishoni mwa wiki.Kulia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
Timu ya soka ya Jukwaa la Wahariri Nchini – TEF na ile ya Wanahabari wa Mkoa wa Iringa leo zimepokea vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki utakaochezwa mwishoni mwa wiki mjini Iringa.
Vifaa vilivyokabidhiwa leo na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim kwa Nahodha wa timu ya Wahariri ambae pia ni Mhariri Mkuu wa Habari wa Gazeti la Mtanzania Kulwa Karedia ni pamoja na jezi seti tatu, viatu, mipira, suti za michezo na soksi.

Akikabidhi vifaa hivyo leo jijini Dar es salaam, Mwalim amesema ni matokeo ya Vodacom kutambua umuhimu wa michezo na namna ambavyo Wahariri wanavyohitaji muda wa kushiriki michezo kwa afya na burudani kutokana na uasili wa majukumu yao ya kila siku.
“Tunafahamu jinsi kazi za Wahariri zilivyo hivyo hii ni fursa nzuri kwao kufanya jambo tofauti ili waweze kuwa na Wakati wa kuburudisha akili nje ya maeneo yao ya kazi tunaamini ni tukio zuri na muhimu kwao”Alisema Mwalim
“Wanahabari wamekuwa wadau wetu wakuu katika biashara hasa pale tunapohitaji kuupasha umma juu ya shughuli zetu mbalimbali hivyo nasi leo tunajisikia furaha kuwezesha tukio lao.” Aliongeza

Mwalim amesema Vodacom inatambua umuhimu wa michezo na ndio maana imekuwa mdau mkubwa wa kuchangia maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini kwenye ngazi mbalimbali kuanzia ligi kuu hadi michezo ya ngazi za chini..
Kwa upande wake Karedia ameishukuru kampuni hiyo kwa kuiwezesha mechi hiyo jambo ambalo linaonesha jinsi kampuni hiyo ilivyo karibu na wanahabari nchini.
“Tunategemea kupata ushindani mkubwa kutoka kwa wanahabari wa mkoa wa Iringa nasi katika kuhakikisha tunatimzia azima ya ushindi timu yangu imekuwa kwenye mazoezi na tunaahidi kubeba zawadi ya ushindi.”Aliongeza

“Tunayofuraha kubwa sana kuona Vodacom ikituunga mkono kutuwezesha mechi yetu ikifana,vifaa hivi tunavipokea kwa furaha na tunaahidi kurudi na ushindi.”Alisema Karedia
Amesema maandalizi ya mechi hiyo yamekamalika na kwamba itafunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt.Christine Ishengoma

Mbali ya kuzipatia vifaa timu zote mbili, Vodacom imetoa pia seti moja ya jezi na mipira minne kwa ajili ya zawadi ya mshindi wa mechi hiyo.
Mbali ya kuidhamini mechi hiyo, Kampuni ya Vodacom imechangia pia Shilingi 12 Milioni kwenye maandalizi ya Mkutano Mkuu huo wa TEF uliopangwa kufanyika kwa siku mbili Oktoba 25 na 26 Mjini Iringa.

0 comments:

Post a Comment

Recent Posts