LEMBELI APOKEA MALALAMIKO YA WADAU WA MSITU WA SAOHILL
Mwenyekiti wa wavunaji Bw. Christian Ahia akisisitiza jambo kwa kamati ya ardhi, maliasili na mazingira, iliyo chini ya mwenyekiti wake mh. Jemsy Lembeli Mbunge. |
Wakilalamikia mgao huo katika kikao baina yao na kamati ya bunge ardhi, maliasili na mazingira, iliyotembelea wilaya hiyo ya Mufindi kwa lengo la kupata taarifa mbalimbali za maeneo ya kazi ya kamati hiyo, nao viongozi wa Wilaya ya Mufindi wanapaza sauti, wakiiomba kamati hiyo kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo mapema.
Dickson Luteleve mwakirishi wa wavunaji amesema gharama za usajili wa kibali zimepandishwa mara tatu zaidi, kutoka tozo la shilingi Laki mbili hadi kufikia laki 7 na elfu 82, wakati mgao wa vibari ukipunguzwa kutoka Qubic mita 500 hadi kufikia Qubic mita 250 pekee.
Mwenyekiti wa wavunaji Christian Ahia ameiomba kamati hiyo kusaidia kutatua changamoto hiyo ambayo alidai kuwa isipoangaliwa kwa jicho la tatu mpango huo unaweza kuchangia uchumi wa wananchi wa Wilaya ya Mufindi kudumaa
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi. Evalister Kalalu amesema amekuwa akipata taabu kwani kimbilio kubwa la wananchi ni katika ofisi yake, na kuiomba kamati hiyo kulitafutia ufumbuzi wa haraka suala hilo kabla halijaleta madhara kwa wananchi.
Naye Mh. Peter Tweve- Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mufindi alisema utaratibu wa kugawa vibari kwa "Qubic mita" sawa kwa waombaji wote pasipo kuangalia uhitaji wa muombaji ni kikwazo kikubwa cha hali ya maendeleo ya wananchi wa wilaya ya Mufindi.
"Ndugu mwenyekiti jambo hili ni shida sasa, kwa ni ugawaji huu haujazingatia hitaji la muombaji, unajua hata hivyi vidole vimetofautiana, kuna vilefu, vinene, vifupi na hata katika utendaji wa kazi vidole hivi vinatofautiana sana, kwa hiyo huu mpango mpya wa kutoa Qubic mita sawa kwa waombaji wote sioni kama hapo mnawatendea haki wananchi wa Mufindi," Alisema Tweve.
Akitoa majibu ya malalamiko hayo, mwenyekiti wa kamati hiyo ya ardhi, maliasili na mazingira mh. Jemsy Lembeli amesema ameyaona mapungufu mbalimbali baada ya kutembelea wilaya hiyo katika sekta ya kamati yake, likiwemo la kutowafikishia wananchi na wadau wa msitu wa saohill utaratibu huo, na kuwa wahusika wamekurupuka kufanya hivyo.
"Niseme hoja zote zilizomo kwenye lisara hii na zile mlizozisema nanyi humu ndani, zote tunazichukua na tutazifanyia kazi immediatilly tukifika tu bungeni, na mrejesho mtauona, lakini niseme jambo hili tumelikisikiahapa ndani kwa mara ya kwanza, Wizara ilishaleta taarifa kwenye kamati, na sisi kama kamati tulishauri wananchi waandaliwe kwanza, waelewe nikwa nini lakini pia wasikilizwe, lakini tunayoyapata hapa ni kuwa wananchi hawajashirikishwa wala hawajaandaliwa vya kutosha juu ya hatua hii, na hatua zote zinazostahili ushirikishwaji hazijafuatwa, mimi ninachomba tuelewane kitu kimoja, haya mtuachieni tutayafanyia kazi, kwani hatuwezi kuwa na majibu hapa ya moja kwa moja,"Alisema Lembeli.
0 comments: