JACKSON KISWAGA AWALIPIA WAKAZI 30 KATIKA MFUKO WA AFYA VIJIJINI CHF
Mkazi
wa kijiji cha Nyamihuu, kata ya Nzihi tarafa ya Kalenga mkoa wa Iringa
Bw. Jackson Kiswaga ametoa msaada wa kulipia kaya 30 katika mfuko wa
afya vijijini (CHF) alioanzishwa na serikali. Amesema amelazimika kutoa
msaada huo baada ya
kuombwa na serikali ya kijiji cha Nyamihuu kusaidia familia zinazoishi
katika mazingira magumu. Wakati wa kukabidhi msaada kwenye kamati ya
kijiji inayoshughulikia masuala ya afya amesema ‘’afya na mali na
utajiri’’ kwa ameipongeza serikali kwa juhudi za makusudi
za kuwapunguzia wananchi mzigi kwa kuanzisha huduma hii ya afya ambapo
kaya moja huchangia asilia 50% na serikali nayo hutoa 50% na kuiwezesha
familia husika kutibiwa kwa mwaka mmoja bure katika zahanati za
serikali.
Mzee
Lasiang’ombe Mbembe mwenyekiti wa CCM kijiji cha Nyamihuu amempongeza
sana Bw. Kiswaga na kumwelezea kuwa na kijana wa kipekee sana. Amesema
kwa miaka kadhaa sasa amekuwa msaaada na mshauri mkubwa kijijini hapo.
Ukiacha msaada baiskeri
aliotoa mwaka juzi kwenye serikali ya kijiji, kuchangia ujenzi wa
nyumba ya waalimu, madawati na kusomesha watoto watatu katika shule ya
kata Kidamili, pia amekuwa akifanya mpango wa upatikanaji wa maji. Mzee
Mbembe amesema ikiwa kijiji kitapata vijana kumi
kama Jackson Kiswaga basi Nyamihuu watakuwa peponi. Yeye mwenyewe
Kiswaga amesema nia yake ni kusaidia familia zote zitakazothibitishwa na
uongozi wa kijiji kuwa hazina uwezo na mpango wake mpana na kusaidia
familia kama 1000 mkoa wote wa Iringa.
Taarifa na Godwin Francis.
0 comments: