Wakati anamwonesa lilipo panga na
kumpa kurunzi Ghati hakujuwa kuwa nini kinafuata alifiki kuwa mambo ya
wanaume pengine anataka kwenda sehemu kwa kuwa ndizo tabia za wanaume wa
maeneo haya kuondoka usiku ama anataka kuangalia mji kama uko sawa
alafu arudi kulala.
" Alipoipata ile panga akaniambia leo
atamitumbua utumbo, akaanza kunipiga kwa panga ile akanijeruhi sikio,
mkono wa kushoto na mguu wa kushoto na kunikata mguu wa kulia ukakatika
kama unavyoona" alieleza kwa masikitiko akiifunua kanga iliyokuwa
amejifunika akiwa amelala kitandani hospitali ya Wilaya Tarime.
Wakati anafanyiwa ukatili huo ali piga
kelele lakini majirani hawakuwahi kufika kumsaidia kwa kuwa ni kawaida
ya mume na mke kugombana na vilio kama hivyo kusikika katika maeneo
hayo.
"Baadaye walikuja na aliposikia
majirani wamefika alikimbia kwa kupitia mlango wa nyuma akitumia
baisikeli yake, majirani walinifunga mguu uliokuwa ukivuja damu na
kunikimbiza katika kituo cha afya Muriba na baadaye kuletwa hapa"
alieleza .
Hata hivyo mwanzoni Ghati alieleza kuwa chanzo cha matatizo hayo yote ni ndoa za mitala na unywaji wa pombe wa mume wake.
" Nimeishi naye kwa miaka mine sasa na
tuna watoto wawili na tulikuwa tunaishi vizuri, tatizo akinywa pombe
huonekana kama amewehuka linguine ni baada ya kuoa mke wa pili ambapo
alianza kunichukia , kuanza kunipiga na sasa kunikata mguu" alisema
Ghati.
Ghati hataweza kurudiana na mume wake
huyo kwa kitendo alichomfanyia kwa vile amesema hakioneshi utu na
kuiomba mahakama imuhukumu mumewe kifungo jera ili ajifunze kutokana
ukatili aliomfanyia.
" Naomba serikali na watu binafsi
wanisaidie magongo ya kutembelea kwa kuwa sasa sina uwezo wa kuyanunua
pia wanisaidie kusomesha watoto wangu maana ni wadogo na mimi ndiye
niliye kuwa nikitafuta tunakula" alisema.
Wananchi walioshuhudia kitendo hicho
walionesha kusikitishwa na kukilaa kuwa kinaendelea kuharibu jina la na
sifa ya Wilaya ya Tarime .
" Sikifurahii kitendo hiki kwani
kinaonesha wazi ukatili wa hali ya juu kwa binadamu mwenzako na hii
inasababisha hata watu ambao hawajawahi kufika huku kutuona sisi ni
wanyama kumbe ni watu wachache wanaotuharibia sifa, mahakama imuhukumu
huyu mtu adhabu kubwa inayomstahili ili liwe fundisho kwa wengine"
alisema Mwita Machera aliyekuwa hostalini hapo.
Jeshi la polisi baada ya kupata
taarifa lilifika lilifika eneo hilo la tukio na kushuhudia kipande cha
mguu kama inavyoonekana kwenye picha hapa na kuamru kizikwe na juhudi za
kumtia nguvuni kuanza.
Hata hivyo siku mojs baadaye Chacha
Mwita alikamatwa na jeshi la polisi kwa kusaidiana na nguvu nza wananchi
ambapo alifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Tarime kujibu mashitaka
hayo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo
kamishina masaidizi wa polisi kanda maalumu ya Tarime (ACP) Justus
Kamugisha lisema kuwa baada ya kuhojiwa Mwiata alikiri kumsababishia mke
wake ukilema wa maisha.
" Vitendo vya kikatili vilishapitwa na
wakati, kumsababishia mtu ukilema wa maisha sii jambo lisilo la utu na
linaonesha kuwa hakuna ubinadamu kwa watu japo si wote" alisema
Kamugisha kwa nija ya simu
HEBU ONA UNYAMA HUU MUME AMKATA MKE WAKE MGUU
Ghati Chacha (21) mkazi wa kijiji cha Nyanitira kata ya Nyansincha Wilayani Tarime amesababishiwa kilema cha maisha kwa kukatwa mguu wake wa kulia na Mume wake baada ya kuchelewa kumfungua mlangao nyakati za usiku.
Akisimulua mkasa huo hivi karibuni akiwa wodi namba sita alikolazwa akiuuguza vidonda na majeraha,Ghati alisema, mume wake aliye mtaja kwa majina ya Chacha Mwita(23) alifika nyumbani saa mbili usiku akiwa amelewa.
"Aliniuliza kwa nini nimechelewa kumfungulia mlango nikamjibu sikuwa nasikia, baadaye akaniomba kurunzi na panga, nikamletea kurunzi na kumwonesha panga lilipo kwa kidole" alisema Ghati.
0 comments: