GLAZERS AKIRI KUCHELEWA KWA MOYES KUNASABABISHA MATOKEO MABAYA MAN UNITED, AAHDI KUMPA SAPOTI YA NGUVU KATIKA USAJILI WA JANUARI

Majanga: David Moyes ameanza vibaya Manchester United WANATAMBUA kwamba klabu ilitakiwa kumnunua Moyes kabla ya mkataba wake na Everton kuisha – iliapate muda wakutosha kufanya usajili wakati wa kiangazi, badala ya kusubiri mpaka Julai 1, siku aliyotakiwa kuanza kazi Old Trafford. Klabu sasa hivi imepania kumpa msaada wote kumaliza tatizo walilokutana nalo wakati wa kiangazi. Wamiliki wa Manchester United, familia ya Glazers wanajipanga kumuunga mkono Moyes wakati wa usajili wa Januari. Man United wanajulikana kwa kutokuwa na tabia ya kutumia fedha nyingi wakati wa Januari, lakini kutokana na mwanzo huu mbaya, imeshawekwa wazi kwamba familia ya Glazer inajipanga kuvunja benki kwa ajili ya beki wa kushoto wa Everton, Leighton Baines na Ander Herrera wa Athletic Bilbao ilikuongeza nguvu kwenye kikosi cha Moyes. Moyes pia atakuwa anajua wazi umuhimu wa kukisuka upya kikosi chake hasa kwenye eneo la baki wa kati. Kichapo cha Jumamosi nyumbani kutoka kwa West Brom kimeifanya United kukamata nafasi ya 12 kwenye ligi. Wamepoteza mechi tatu kwenye msimu huu wa ligi tayari na Moyes amekiri kwamba hana wachezaji wa kiwango cha dunia wa kutosha. United leo wanaenda Ukraine leo kwa ajili ya mechi ngumu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Shakhtar Donetsk. Moyes tayari anajivunia kushinda mechi ya kwanza ya dhidi ya Bayer Leverkusen, lakini hataki kupoteza mechi nyingine kuelekea kwenye mechi ya Jumamosi dhidi ya Sunderland. Nyuma ya pazia pale Old Trafford, Moyes anaungwa mkono na viongozi wakubwa wa Man United.
Wanaweza: Mwenyekiti Joel (kulia) na Avram Glazer wamiliki wa United Kocha alikiri wiki iliyopita kwamba Man United walishindi ligi kuu msimu uliopita kwa sababu kulikuwa hakuna upinzani wa kweli. Familia ya Glazers na Mtendaji Mkuu wa United, Ed Woodward wanakubali kwamba kikosi ambacho Moyes amerithi kutoka kwa Sir Alex Ferguson hakina uwezo wa kuchukua ubingwa na baada ya kuwakosa Baines na Herrera, United wataangalia uwezekano wa kutoa ofa nyingine kwa ajili yao baada ya mwaka mpya. Beki wa zamani wa United, Gary Neville amesisitiza Moyes atapewa muda wa kutosha licha ya kuanza msimu vibaya. Akizungumza na Sky Sports, Neville alisema: “kwa sasa watakuwa wanaangalia tatizo nini na watahitaji kujituma na kumaliza tatizo hilo. Nilisema mwanzo wa msimu kwamba wachezaji watakuwa na changamoto kubwa sana.
Imani: Gary Neville anaamini Moyes atapewa muda wa kuthibitisha ubora wake Old Trafford “Je wanaweza kucheza bila ya Sir Alex Ferguson? Siyo David Moyes pekee ambaye anaumia, kuna wachezaji wengi pale wenye uzoefu mkubwa ambao pia wanaumia sana. Unafikiri namna Sir Alex Ferguson, alipewa muda wa miaka mitatu au minne kutengeneza timu, alikuwa kwenye presha kwa asilimia 100. “David Moyes, hakuna ubishi kwamba bado anajitahidi kuzoea kazi yake, kuwajua wachezaji, utamaduni na jinsi ya kuzungumza na waandishi wa habari. “Kuna kitu kimoja kiko wazi. Una Sir Bobby Charlton kwenye bodi yako, una David Gill. Huyu jamaa haendi kokote. Unampa miaka mitatu au minne kutengeneza klabu.”
Uvumilivu: Sir Alex Ferguson na Sir Bobby Charlton wanajipanga kumpa Moyes muda anautaka Ukiachana na Bodi, Moyes anatakiwa kutafuta njia ya kuwafanya wachezaji wajitoe kwa kila kitu. Kushindwa kufanya vizuri kwa wachezaji wengi wa kimataifa katika mechi dhidi ya West Brom na Manchester City mwezi uliopita hakuna ubishi kwamba kunatatizo kwenye mbinu za Moyes. Kuna taarifa kwamba wachezaji wa United wamekuwa wakifanya mazoezi vizuri, hatahivyo kuna maswali juu ya mazoezi magumu yanayotolewa na kocha huyo. Wakati ambao wachezaji kama Wayne Rooney wakifurahia mazoezi ya Moyes, wengine wameshangazwa. Lakini kocha huyo anaamini kwamba ipo siku mazoezi yake magumu yataanza kulipa tu Tabasamu: Wayne Rooney (kulia) akifurahia mazoezi ya Moyes lakini wachezaji wengine wameshangazwa
Kumekuwa na madai kutoka kwa kocha wa makipa wa zamani wa United, Eric Steele, kwamba Moyes alikataa ushauri wa Ferguson kubaki na wasaidizi wake, huku pia kukiwa na taarifa kwamba msaidizi wa Fergie Rene Meulensteen — alikataa kufanya kazi chini ya Moyes. Kuhusiana na wachezaji wake Moyes amekiri kwamba bado anawasoma wengine, inashangaza kuona kuna dalili za Shinji Kagawa kuondoka Old Trafford.

0 comments:

Post a Comment

Recent Posts