FUMANIZI LA AIBU IRINGA, ALIYEFUMANIWA ADAI ALIPIMA UKIMWI KABLA
Njemba linalotuhumiwa kuvunja amri na mke wa mtu likiwa limelama kitandani huku likiomba msamaha kwa kosa hilo |
Hapa njemba hilo likiwa bado limejilaza kitandani kwa mke wa mtu |
Polisi wakimshusha kitandani mtuhumiwa huyo |
Mgambo na wananchi wakiwa wameweka ulinzi sawa mlangoni |
Hapa polisi wakimtoa mtuhumiwa wa fumanizi ndani ya nyumba |
gari la polisi likijiandaa kuondoka eneo la tukio |
Kijana mwenye mke Bw Kilave kulia akishusha usafiri wake wa Baiskeli iliyotumika kwenda kufanya fumanizi asubuhi ya leo |
Add caption |
ASKARI polisi mjini Iringa
wamefanikiwa kuokoa maisha ya njemba mmoja mkazi wa Ilala mjini
Iringa aliyefumaniwa asubuhi ya leo kwa tuhuma za kuvunja amri ya
sita na mke wa mtu katika chumba cha wanandoa hao.
Njemba
hilo lililofumaniwa limejitambulisha kwa jina na Gilberty Mapunda
(35) mzaliwa na Manda wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe ila kwa sasa
ni mkazi wa Ilala mjini hapa.
Tukio
la kufumaniwa kwa njemba hilo limetokea majira ya saa 12.30
asubuhi ya leo baada ya mume wa mwanamke aliyefumaniwa kufika
ghafla eneo la Mkwawa jirani na klabu cha pombe za kienyeji cha
Mapinduzi ambako ni nyumbani makazi ya mwanamke huyo .
Hata
hivyo katika hali ya kushangaza ni pale njemba hilo kutaka
kumshikisha adabu mwenye mke kwa madai kuwa mwanamke huyo
alimweleza kuwa hana mume na mume aliyekuwa nae ni ana mke wake
hivyo hakuona kosa yeye kumsaidia kumpa huduma mwanamke huyo ambae
alikuwa akionyesha kumpenda zaidi .
"
Mimi kaka kweli nilidanganywa na mke wako kuwa wewe una mke
mwingine hivyo haotafika nyumbani hapo ....lakini naomba unisamehe
ama tumalizane kwani tambua kuja kwangu hapo ni kukusaidia kutoa
huduma kwa mke wako ambae mimi amenipenda pia"
Pia alisema kuwa kuhusu kuambukizana UKIMWI asiwe hofu ya kumtazama wembamba wake kuwa ni mtu aliyeathirika .
"
Kaka naomba unielewe hii afya yangu ya wembamba isikutishe na
kunipa adhabu kubwa ukajua nimeathirika hapana hii ni afya yangu ya
kawaida .....kama UKIMWI mimi nimetoka kupima juzi tu nipo salama
kabisa kwa hilo ondoa shaka"
Mume
wa mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Kilave alisema
kuwa mke wake anaitwa Beatrice Kisia amepata kuzaa nae wawili
akiwemo mmoja wa kike na mwingine wa kiume na hata nyumba hiyo
ambayo leo amemfumania mwanaume huyo ni nyumba ambayo ameijenga yeye
kwa ajili ya familia yake hiyo .
Alisema
kuwa mtuhumiwa wa fumanizi hilo anatambua vema kama mwanamke huyo
ni mke wake na kila wakati wamekuwa wakipishana akipeleka huduma .
Kilave
alisema kuwa jemba hilo baada ya kuingia katika chumba chake
walilazimika kumtoa mtoto mdogo ambae ni mgonjwa na kumpeleka
chumba cha pili alichokuwa amelala bibi wa mtoto na wao kuamua
kukitumia kitanda hicho kwa mambo yao.
Pia
alisema mwanamke baada ya kuona hali ni tete baada ya fumanizi
alilazimika kufungua mlango na kukimbia nje na kumuacha mtuhumiwa
huyo akiendelea kulala kabla ya kufungiwa katika chumba hicho hadi
polisi walipofika na kumchukua .
Jeshi
la polisi mkoa wa Iringa limethibitisha kuwepo kwa tukio hilo
na kupongeza hatua ya mwanaume huyo kutochukua sheria mkononi .
0 comments: