Home
» Enterteinment
» Forbes Africa & Channel O watoa orodha ya wasanii 10 wa Afrika wanaoingiza mkwanja zaidi
Forbes Africa & Channel O watoa orodha ya wasanii 10 wa Afrika wanaoingiza mkwanja zaidi
Kwa mara ya kwanza jarida la Forbes Africa limeshirikiana na
kituo cha runinga cha Afrika Kusini cha Channel O kupitia kipindi chake cha Top
Ten Most kupata orodha ya kwanza na ya uhakika ya wasanii 10 wa Afrika
wanaoingiza mkwanja zaidi, Top
Ten Mosy Bankable African Artists.
Kuwepo kwa Akon kwenye list hii kunaleta utata mkubwa hasa
kwakuwa utajiri wake mwingi umetokana na biashara anazozifanya akiwa Marekani,
tofauti na wasanii wengine kwenye list ambao pesa zao zote zinatokana na mambo
wanayoyafanya barani Afrika. Hiyo ni kama kuwaonea wasanii wenye makazi yao
Afrika. Hata hivyo kwa mujibu wa Forbes, utajiri wake unazidi dola milioni 80.
2. Don Jazzy – Nigeria
Utajiri wa Don Jazzy unatokana hasa na madeal ya matangazo na
mikataba na makampuni kama Samsung , MTN, Loya Milk na mengine. Mwaka huu
alitengeneza wimbo rasmi wa Samsung AFCON2013.Baada ya kuvunjika kwa uhusiano
wake na D’Banj na kupelekea kufa kwa Mo’ Hits, producer huyo alifungua record
label nyingine, Mavin Records na kusaini wasanii kadhaa akiwemo Tiwa Savage.
Pamoja na hivyo pia, Don Jazzy ana miradi kibao kama ya club za starehe,
nyumba, kampuni ya nguo na zingine.
3. P-Square
Pesa za mapacha hawa zinatokana zaidi na tour zisizo na mwisho.
Ni wasanii wanaochaji pesa nyingi zaidi kwa show moja. Mwaka jana walikuwa na
ziara kwenye nchi nyingi za Afrika ambako waliingiza mkwanja mrefu kiasi cha
kumfanya Peter Okoye anunue nyumba ya kifahari nchini Marekani. Licha ya kuwa
na nyumba yao nyingine ya kifahari nchini mwao iitwayo Squareville, wasanii hao
wanajenga mjengo mwingine wa hatari ambao unakaribia kumalizika. Deal lao na
kampuni ya Glo limewaaingiza karibu shilingi bilioni 1 kila mwaka. Kwa sasa
wapo kwenye ziara ya Marekani na Canada.
4. D’Banj
Pamoja na kuingiza fedha nyingi kutokana na pesa kubwa
anazochaji kwenye show zake (N2.6m kwa show), D’banj hujihusisha pia na
biashara kama reality show ya Koko Mansion, Koko Lounge ya Lagos na Uingereza,
Koko Foundation na Koko Mobile.
Ameshadaka madeal kibao ya matangazo ikiwa pamoja na mkataba wa
naira milioni 30 na kampuni ya Virgin Colours, N25m za Virgin airline, N20m za
Nutricima na deal la Globacom, na mkataba wa N100m na UAC. Aliingiza mkwanja
mwingine mrefu kwa kushiriki kwenye kampeni ya Rais Goodluck Jonathan. Mwezi
June mwaka huu alipata deal nono na kampuni ya Etisalat la N250m.
5. Wizkid
Kukamata namba tano kwa Wizkid ni surprise kwa wengi hasa
kwakuwa hana muda mrefu kihivyo kwenye muziki. Wizkid aliingiza dola 350,000
kutokana na deal la Pepsi na pia deal la N50m kutoka kwa MTN. Show anazofanya
zinamuingiza fedha nyingi zaidi.Chanzo kingine cha mapato ni mauzo ya nyimbo
zake.
6. 2 Face
Pamoja na muziki ambapo huchaji dola 500,000 hadi 800,000 kwa
show, 2 Face amekuwa akiingiza fedha nyingi kutokana na mikataba ya matangazo
kama ya Guinness na Airtel ambayo yote kwa pamoja aliingiza N42m. Ana miliki
pia night club. Pia aliingiza N30m za ‘Phat Girlz’. Kwa sasa amewekeza zaidi
kwenye biashara ya makazi zinazofikia thamani ya N2.7m
7. Anselmo Ralph
7. Anselmo Ralph
Anselmo Ralph Andrade Lamb ni msanii mkubwa wa Angola. Ni
muimbaji R & B, Soul na Kizomba. \
8. Sarkodie
Rapper Sarkodie kutoka Ghana ni mjasiriamali mzuri kwani hadi
sasa ameshaanzisha miradi kibao ikiwemo simu zake za mkononi, nguo, maji ya
kunywa na mingine. Utajiri wake mkubwa umefanya watu wamhisi ni member wa
Illuminati.
9. Ice Prince
9. Ice Prince
Mwaka huu Ice Prince alikataa deal nono la kampuni ya Glo na
kila mmoja akagundua ni kwa kiasi gani rapper huyo ana fedha kiasi cha kukataa
deal kama hiyo. Inasemekana alitaka alipwe dola milioni 1. Pesa zake nyingi
zimetokana na show anazofanya na pia amekuwa balozi wa One Campaign kwa muda.
10. Banky W
10. Banky W
Bankole Wellington mmiliki wa EME records, ndiye aliyemsaidia
Wizkid kufika hapo alipo leo. Ameshasaini mikataba ya matangazo na makampuni
mengi kama Samsung Electronics West Africa ambao walimlipa $890,000. Banky W
alishawahi pia kuwa balozi wa Etisalat na Coca Cola.