Wasichana 2 waliomwagiwa Tindikali Zanzibar wawasili kwao Uingereza
Katie na Kirstie |
Mama mwenye hasira wa mmoja wa wasichana wa Uingereza
waliomwagiwa acid mjini Zanzibar ameungana na bintiye nchini humo baada ya leo
kuwasili kwa ndege kwenye hospitali kwaajili ya matibabu.
Mama huyo, Nicky Gee alionekana kushindwa kujizuia kulia baada
ya kumuona binti yake Katie na rafiki yake Kirstie Trup wakishuka kwenye
ambulance akiwa amefunikwa blanket.
Wasichana hao ambao wote wana miaka 18 walipelekwa kwenye
hospitali ya Chelsea and Westminster kutibiwa haraka majeraha ambayo baba yake
Katie ameyaita mabaya yasiyoelezeka.
Wote wameungua vibaya baada ya kumwagiwa tindikali usoni wakati
walipokuwa wakiingia kwenye mgahawa mjini Zanzibar. Hilo lilikuwa shambulizi la
tatu wakati walipokuwa visiwani humo. Awali mmoja wa wasichana hao
alishambuliwa na msichana wa kiislam baada ya kumsika akiimba wimbo wakati wa
mwezi wa Ramadhan.
Polisi wamedai kuwa washukiwa saba akiwemo muongozaji wa watalii
wamekamatwa jana asubuhi.Na sasa zawadi ya paundi £4,000 imetangazwa kutolewa
na polisi Zanzibar kwa atakayesaidia kupatikana kwa kwa wahalifu hao.
Marafiki wanadai kuwa walikuwa wamelengwa kushambuliwa kwasababu
walikuwa ni wayahudi na polisi wanadai kuwa walikuwa wanataka kuongea na
mhubiri wa kiislam ambaye huenda ndiye alipanga shambulizi hilo.Polisi wamedai
kutoa warrant ya kukamatwa kwa Sheikh Issa Ponda Issa, ambaye inasemekana
mafundisho yake yamechochea mashambulizi hayo ya tindikali.
Wasichana hao watapata matibabu ya kina kutokana na mejeraha
waliyoyapata kwa kumwagiwa tindikali hiyo iliyomwagika usoni, kifuani, miguuni
na mgongoni.
Katie baada ya kumwagiwa tindikali |
Mikono yao pia imejeruhiwa kwakuwa walikuwa wakijaribu kufuta
tindikali hiyo. Baba yake na Miss Trup, Marc, 51, milionea na daktari wa meno
alisema mpita njia alienda kuwasaidia wasichana hao baada ya kushambuliwa na
alimpigia simu.
Marafiki hao walikuwa wameenda Zanzibar kama walimu wa kujitolea
kwenye kituo cha watoto yatima.
Tukio hilo linaweza kuathiri vibaya sekta ya utalii visiwani
Zanzibar.
“This does wonders for the tourism industry in Zanzibar,
obviously they don’t need the money!! Hope the girls get thru this horrible
incident,” ameandika msomaji mmoja kwenye mtandao wa Daily Mail.
‘Really wanted to book a holiday in Zanzibar, not anymore,’
ameandika mwingine aitwaye, Sassy1.
You may also Like
Followers
Tags 2
Popular Posts
-
New AUDIO | Geez Mabovu - Story | Download Sikiliza & Download Nyimbo ya Marehemu GEEZ MABOVU akiwa amemshirikisha GALATONE