Picha zaidi za namna Feza Kessy alivyopokelewa Gaborone, Botswana
Feza Kessy ameshakuwa staa wa Afrika. Namna ambavyo amekubalika
nchini Botswana aliko mpenzi wake O’neal si kitu cha kawaida. Feza amepata
mapokezi ya kipekee nchini humo kiasi kilichowalazimu yeye na mpenzi wake
wazunguke mitaa ya mji mkuu, Gaborone iliyokuwa imefurika mashabiki wake
kumtazama na wao wakiwa kwenye gari la wazi wakiwasalimia kwa furaha kubwa.