Wasanii 5 wa Hip Hop wenye mkwanja zaidi – 2013: The Forbes Five
Hakuna ubishi kuwa Diddy sio rapper mwenye uwezo wa kushtua
lakini anajua kutengeneza mshiko. Ni mjasiriamali wa muziki na ndio maana mwaka
huu ameongoza list ya jarida la Forbes la wana Hip Hop wenye mkwanja mrefu
zaidi.
Kwa mujibu wa ‘Forbes Five’ orodha ya wasanii wa hip hop
wenye mkwanja zaidi, Diddy ambaye ni mwanzilishi wa Bad Boy Records ana utajiri
ufikao dola milioni 580. Utajiri wake unatokana na nini? Fedha nyingi inatokana
na biashara yake nje ya muziki kama deal la kilevi maarufu cha Ciroc na
biashara zingine kibao.
Namba mbili imeenda kwa Shawn “Jay-Z” Carter, ambaye
ameachwa mbaaaaaaaali na Diddy akiwa na utajiri ufikao dola milioni 475.
Hov anaendelea kuingiza mkwanja toka deal la milioni 204 la
mauzo ya Rocawear mwaka 2007 na mkataba wake wa dola milioni 150 na Live Nation
mwaka uliofuatia. Bado ana hisa kwenye label ya Roc Nation
pamoja na timu ya
kikapu ya Brooklyn Nets na uwanja wa Barclays Center pia. Michongo mingine
inayompa mkwanja ni pamoja na ushirikiano na Duracell, Budweiser na D’ussé
Cognac.
Nafasi ya tatu imechukuliwa na mchawi wa beats, Andre “Dr.
Dre” Young akiwa na utajiri wa dola milioni
350. Yeye ashukuru sana mafanikio ya headphones zake za Beats by Dr. Dre.
350. Yeye ashukuru sana mafanikio ya headphones zake za Beats by Dr. Dre.
Mkataba wake na kampuni ya simu ya HTC uliompa dola milioni
300 August 2011, umeendelea kuwa mnono baada ya Beat by Dre kushikilia asilimia
65 la soko la headphones duniani.
Bitoz wa nguvu Bryan “Birdman” Williams amekamata nafasi ya
4. Akiwa mkuu wa himaya ya Cash Money/Young Money jamaa ana utajiri ufikao dola
milioni 150.
Nafasi ya mwisho inakamatwa na Curtis “50 Cent” Jackson
mwenye dola milioni 125.
Huyu ni master mwingine wa kutengeneza brand na zikafanya
vizuri. Pesa nyingi aliyonayo inatokana na mauzo ya muziki wake, michongo
mbalimbali video games na vitabu. Pia hisa alizonazo kwenye brand kama
VitaminWater na mauzo ya headphones zake, SMS Audio.
0 comments: