Diamond kamjengea mama yake nyumba ya shilingi milioni 260
Karibu kila mtu anayeufuatilia muziki
wa Bongo Flava anajua Diamond ndio msanii anayetafutwa zaidi kwaajili ya show
kuliko msanii yeyote Tanzania but nani alifahamu kuwa amemjengea mama yake
nyumba yenye thamani ya shilingi milioni 260?
Lakini hivyo ndivyo alivyofanya msanii
huyu kipenzi cha kinadada kwa mujibu wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM
kama alivyofunguka jana.
Na kwa mujibu wa interview aliyoifanya
hivi karibuni kwenye kipindi kingine cha XXL katika kituo hicho cha radio,
hitmaker huyo wa Mawazo yuko booked hadi mwezi July.
“Mtu anasema yeye ananiroga mimi
nashuka mwezi mzima ntakuwa na show Europe, Jumamosi nina show Hyatt pale,
Jumapili nina show Mombasa wiki inayofuata ninasafiri naenda nje nina show kama
kumi yaani ukinibook mimi mpaka mwezi wa saba nimejaa wewe unaniambia mimi
nimeshuka vipi,” alisema Diamond.
0 comments: